• HABARI MPYA

  Jumamosi, Juni 24, 2017

  MMOJA TU ‘APIGWA CHINI’ UCHAGUZI WA TFF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemuengua mgombea wa nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu Dodoma.
  Kamati hiyo imewapitisha wagombea wengine wote 12 baada ya kumuengua Abdallah Mussa aliyekuwa anawania nafasi ya Ujumbe kutoka Kanda namba moja inayohusisha mikoa ya Kagera na Geita kwa sababu hakuambatanisha kivuli cha cheti chake cha kidato cha Nne kwa mujibu wa kanuni ya 9 inayozungumzia sifa nane za kuwania uongozi TFF. 
  Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amesema leo kwamba, wagombea 10 wamepitishwa kuwania nafasi ya Urais, sita Umakamu wa Rais na 57 kwa Ujumbe wa Kamati ya Utendaji kupitia Kanda mbalimbali.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi atetetea nafasi yake dhidi ya wagombea tisa Agosti 12 mjini Dodoma

  Lucas amesema kwamba wagombea wote wanatakiwa kufika kwenye usaili utakaofanyika kuanzia Juni 29 hadi Julai 1, mwaka huu katika ofisi za TFF zilizopo Uwanja wa Karume mjini Dar es Salaam.
  “Wafike kuanzia saa 4:00 asubuhi wakiwa na nyaraka halisi za viambatisho vyote walivyoweka kwenye fomu za maombi. Vyeti vya elimu ya Sekondari viwe vya Baraza la Mitihani (NECTA),”amesema Lucas.
  Waliopitishwa ni Ally Mayay, Athumani Nyamlani, Frederick Mwakalebela, Jamal Malinzi, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, John Kijumbe, Shija Richard na Emmanuel Kimbe kwa nafasi ya Urais.
  Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa. na Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kwa nafasi ya Umakamu wa Rais.
  Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kutoka Kanda namba 1, Mikoa ya Kagera na Geita; Salum Chama, Kaliro Samson na Leopold 'Taso' Mukebezi, Kanda namba 2 Mikoa ya Mara na Mwanza; Vedastus Lufano, Ephraim Majige, Samuel Daniel na Aaron Nyanda na Kanda namba 3 mikoa ya Shinyanga na Simiyu; Benista Rugora, Mbasha Matutu na Stanslaus Nyongo.
  Kanda namba 4 mikoa ya Arusha na Manyara; Omari Walii, Sarah Chao na Peter Temu, Kanda namba 5 mikoa ya Kigoma na Tabora; John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael, Kanda namba 6 mikoa ya Katavi na Rukwa; Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo.
  Kanda namba 7 mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa; Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava, Erick Ambakisye na Abousuphyan Silliah, Kanda namba 8 mikoa ya Njombe na Ruvuma; James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela na Kanda namba 9 mikoa ya Lindi na Mtwara; Athuman Kambi na Dunstan Mkundi.
  Kanda namba 10 mikoa ya Dodoma na Singida ni Hussein Mwamba, Mohamed Aden, Mussa Sima, Stewart Masima, Ally Suru na George Benedict, Kanda namba 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro ni Charles Mwakambaya, Gabriel Makwawe, Francis Ndulane na Hassan Othman ‘Hassanol’. 
  Kanda namba 12 mikoa ya Kilimanjaro na Tanga; Khalid Mohamed, Goodluck Moshi na Thabit Kandoro, Kanda namba 13 mkoa wa Dar es Salaam; Emmanuel Ashery, Ayoub Nyenzi, Saleh Alawi, Shaffih Dauda, Abdul Sauko, Peter Mhinzi, Ally Kamtande, Said Tully, Mussa Kisoky, Lameck Nyambaya, Ramadhani Nassib, Aziz Khalfan, Jamhuri Kihwelo, Saad Kawemba na Bakari Malima.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MMOJA TU ‘APIGWA CHINI’ UCHAGUZI WA TFF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top