• HABARI MPYA

  Thursday, July 06, 2017

  FERNANDO TORRES ASAINI MKATABA MPYA NA ATLETICO MADRID

  MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Fernando Torres amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kubaki mji mkuu wa Hispania  hadi Juni 2018.
  Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga imesema jana katika taarifa yake kwamba imemuongeza mkataba mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea.
  "Nina furafa kubaki hapa kwa mwaka mwingine,"amesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33, Torres, ambaye alijiunga na Atletico akiwa ana umri wa miaka 11 na amecheza jumla ya mechi 294.
  Alipewa nafasi kucheza kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha kwanza mwaka 2001, na baadaye akawa Nahodha kabla ya kutimkia Liverpool mwaka 2007.
  Akacheza pia Chelsea na AC Milan kabla ya mshindi huyo wa mataji mawili ya Uaya na Kombe la Dunia mwaka 2010 kurejea Atletico mwaka 2015.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: FERNANDO TORRES ASAINI MKATABA MPYA NA ATLETICO MADRID Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top