• HABARI MPYA

    Tuesday, July 04, 2017

    STRAIKA CHIPUKIZI WA BURUNDI ASAINI MIAKA MITANO MAN UNITED

    KLABU ya Manchester United imemsajili mchezaji mzaliwa wa Burundi, mshambuliaji chipukizi Largie Ramazani.
    Baada ya kuzaliwa Burundi, Ramazani alikwenda kujiunga na akademi ya Anderlecht ya Ubelgiji kabla yaa kuhamia Charlton Athletic ya England.
    Kinda huyo wa umri wa miaka 16 aliwasili viwanja vya mazoezi vya United, Carrington jana kuanza maandalizi ya msimu.
    Inafahamika kwamba Ramazani amejiunga na klabu kwa mkataba wa miaka minne baada ya kuwavutia wasaka vipaji wa klabu hiyo. 
    Mshambuliaji chipukizi wa Burundi, Largie Ramazani akiwa ameshika jezi ya Manchester United baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano

    Mwandishi wa Habari wa Ubelgiji, Kristof Terreur ametweet picha ya Ramazani akiwa ameshika jezi ya United baada ya kukamilisha uhamisho huo.  
    United inaendelea kuimarisha timu yake ya vijana kwa Mbelgiji huyo kujiunga nao akiwafuatia wapya wengine akina Aliou Badara Traore na Ethan Galbraith. 
    Traore ametokea PSG ya Ufaransa na amesaini mkataba wa miaka minne, wakati Northern Irishman Galbraith amesaini mkataba wa miaka mitatu. 
    United inatumai wachezaji hao watakuja kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha kwanza cha Jose Mourinho baadaye.
    Kwa sasa, Mreno huyo anakwenda mbio kuhakikisha anawasajili wachezaji wa kiwango cha dunia, akiwemo mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata ambaye anamuhitaji zaidi kuimarisha safu yake ya mbele.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STRAIKA CHIPUKIZI WA BURUNDI ASAINI MIAKA MITANO MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top