• HABARI MPYA

    Sunday, July 09, 2017

    MWAKYEMBE AWATAKA STARS WAJIPANGE KUING’OA RWANDA CHAN

    Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
    WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amewataka wachezaji timu ya soka ya taifa Tanzania, Taifa Stars kuelekeza nguvu katika mchezo dhidi ya Rwanda ili waitoe na kusonga mbele kwenye michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), baada ya mafanikio ya Kombe la COSAFA.
    Taifa Stars imewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo alfajiri ikitokea Afrika Kusini, ambako walishiriki mashindano ya Kombe la COSAFA na kumaliza katika nafasi ya tatu.
    Na katika mapokezi ya timu hiyo
    Waziri Mwakyembe (katikati) akiwa na baadhi ya wachezaji wa Taufa Stars wakati wa mapokezi leo Alfajiri JNIA

    Timu Mwakyembe alikuwepo katika mapokezi ya timu hiyo majira ya saa 9 na ushei usiku JNIA sambamba na Kaimu Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia na akawapongeza kocha Salum Mayanga na wasaidizi wake pamoja na wachezaji kwa mafanikio hayo.
    “Nakuchua fursa hii kuwapongeza kwa kutupa heshima katika nchi yetu kwa hatua mliyofikia, nina furaha sana na karibuni tena nyumbani na ninwaomba muelekeze nguvu zenu katika mashindano yajayo, ili kuiletea nchi yetu maendeleo katika soka,”alisema Mwakyembe.
    Kwa upande wake, kocha Mayanga amesema kwamba wanamshukuru Mungu kwa mafanikio hayo na sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo dhidi ya Rwanda kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa Afrika (CHAN).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWAKYEMBE AWATAKA STARS WAJIPANGE KUING’OA RWANDA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top