• HABARI MPYA

  Thursday, July 13, 2017

  MTIBWA SUGAR MAPEMAA ‘WANALIAMSHA DUDE’ HAPA HAPA DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Baram Mtibwa Sugar wanatarajiwa kuingia kambini Jumapili wiki hii mjini Dar es Salaam kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya.
  Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu 1999 na 2000 enzi hizo yeye akiwa mchezaji wa timu hiyo, Zuberi Katwila amesema kwamba huu ni wakati mwafaka kuingia kambini kwa sababu Ligi Kuu inaanza mwezi ujao.
  “Nadhani huu ni wakati mwafaka kwa timu kwenda kuanza maandalizi, kwa sababu Ligi Kuu itaanza mwishoni mwa Agosti, kwa hivyo kipindi hiki tunataiwa kukitumia vizuri kwa kuiandaa timu vyema,”alisema Katwila jana.
  Kwa upande wake, Mkurugenzi na Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser alisema kwamba wamewasiliana na wachezaji wote kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao na kuingia kambini mapema kutawasaidia wachezaji kutengeneza muunganiko mzuri katika timu kwa wachezaji wapya kuendana na falsafa ya klabu.
  Pamoja na timu kwenda kambini, Bayser pia amesema zoezi la usajili bado linaendelea kwa kusajili wachezaji wapya kuimarisha zaidi kikosi.
  Na amesema kambi ya mazoezi itaanzia Dar es Salaam kwa wiki mbili kabla ya kurejea maskani yao, Manungu, Turiani, mkoani Morogoro kuendelea na maandalizi zaidi.
  Mtibwa Sugar inatarajiwa kuuanza msimu kwa kuwania Kombe la Faith Baptist kwa kumenyana na Mbeya City Uwanja wa Jamhuri, Morogoro Julai 29, mwaka huu. Mtibwa Sugar ni mabingwa wa mara zote mbili wa Faith Baptist tangu ianzishwe na ni matarajio yao kutwaa tena.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR MAPEMAA ‘WANALIAMSHA DUDE’ HAPA HAPA DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top