• HABARI MPYA

  Friday, July 07, 2017

  MAMIA WAMSINDIKIZA SHAABAN DEDE SAFARI YAKE YA MWISHO

  MAZISHI ya mwimbaji mkongwe wa Msondo Ngoma, Shaaban Dede aliyefariki dunia jana asubuhi, yamefanyika leo saa saba mchana na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa Dar es Salaam. 
  Mwimbaji huyo aliyetesa kwa sauti yake tamu na kwa tungo zake za kusisimua, amezikwa katika makaburi ya Kisutu huku idadi kubwa ya wanamuziki wa fani mbalimbali ikiwa sehemu ya umati uliofurika makaburini hapo. 
  Aidha, Dede pia amezikwa na vigogo wengi wa dini ya Kiislam, maofisa wengi wa serekali na wanamichezo maarufu. 
  Watu wakiwa wamebeba jeneza la mpendwa wao, Shaaban Dede Adhuhuri ya leo kwenda kumpumzisha katika nyumba yake ya milele PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  Pengine kwa miaka ya hivi karibuni, ukiondoka msiba wa marehemu Muhudini Gurumo, hakuna tena msiba wa mwanamuziki wa dansi uliohudhuriwa na watu wengi kama huu wa Dede.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMIA WAMSINDIKIZA SHAABAN DEDE SAFARI YAKE YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top