• HABARI MPYA

  Friday, July 14, 2017

  JERRY MURO ‘APIGWA CHINI’ RASMI YANGA, JAMAA WA MBEYA CITY ACHUKUA NAFASI

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KATIBU Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa leo amemtambulisha Dissmas Ten kuwa Ofisa wa Habari wa nne wa klabu hiyo tangu mwaka 2010, akichukua nafasi ya Jerry Muro anayeondoka baada ya kumaliza mkataba wake.
  Louis Sendeu alikuwa Ofisa Habari wa kwanza wa Yanga mwaka 2010 chini ya Mwenyekiti, Wakili Imani Mahugila Madega na akaendelea na kazi hadi chini ya Mwenyekiti Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kabla ya kuondolewa kufuatia kuingia madarakani kwa Mwenyekiti Yussuf Manji.
  Baraka Kizuguto akakaimu kwa muda nafasi hiyo, kabla ya naye kuondolewa na kuingia Muro ambaye hata kabla ya kumaliza mkataba wake, alifungiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa makosa ya kimaadili.
  Dissmas Ten akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jangwani baada ya kutambulishwa, huku Charles Boniface Mkwasa (kulia) akimsikiliza. Kushoto ni Godlisten Anderson 'Chicharito'
  Wapenzi wa Yanga wakifuatilia mkutano huo kupitia dirisha la ukumbi wa mikutano wa klabu

  Na siku chache baada ya kumaliza adhabu yake, Muro anaondolewa kazini na nafasi yake ikichukuliwa na Ten, aliyekuwa Ofisa Habari wa klabuya Mbeya City ya Mbeya.
  Katika mkutano na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Ten ameahidi kuleta mapinduzi katika Idara ya Mahusiano na Mawasiliano ya Yanga.
  Amesema anataka kuifanya Idara hiyo iwe moja ya vyanzo vya mapato vya klabu kupitia akaunti zake mbalimbali za mitandao ya kijamii.
  Na Mkwasa akasema Ten atafanaya kazi na Godlisten Anderson ‘Chicharito’, ambaye alikuwa anafanya shughuli za Idara hiyo kipindi chote cha mwaka mmoja uliopita kufuatia kufungiwa kwa Jerry Muro.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JERRY MURO ‘APIGWA CHINI’ RASMI YANGA, JAMAA WA MBEYA CITY ACHUKUA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top