• HABARI MPYA

  Monday, July 03, 2017

  EVERTON YASAJILI BEKI LA MAN UNITED PAUNI MILIONI 30

  KLABU ya Everton imeendelea kumwaga fedha kusajili kujijenga kwa msimu ujao, baada ya leo kukamilisha uhamisho wa beki wa kati wa zamani wa Manchester United, Michael Keane kutoka Burnley kwa ada ya uhamisho ya rekodi, Pauni Milioni 30.
  Beki huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini mkataba wa miaka mitano kuhamishia kazi zake Uwanja wa Goodison Park.
  Na Keane anakuwa mcheaji wa tano kusajiliwa na kikosi cha kocha Ronald Koeman katika dirisha hili la usajili, kuashiria timu hiyo inayodhaminiwa na SportPesa imedhamiria 'kujiumba upya'. 

  Everton imemsajili beki wa kati wa zamani wa Manchester United, Michael Keane kutoka Burnley kwa dau la Pauni Milioni 30 PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  Keane anasajiliwa Everton baada ya timu hiyo ambayo wiki ijayo itakuja Tanzania kucheza na Gor Mahia ya Kenya kuwsajli pia kipa Jordan Pickford, kiungo Davy Klaasen na washambuliaji Sandro Ramirez na Henry Onyekuru ambao kwa pamoja wanafanya klabu hiyo itumie jumla ya Pauni milioni 96 kusajili.
  Manchester United inatarajiwa kupata hadi Pauni Milioni 7.5 katika dili hilo, ikiwa ni asilimia 25 ya mauzo baada ya makubaliano wakati Keane anaondoka Old Trafford kwenda Burnley mwaka 2015. 
  Kocha wa Toffees, Koeman anaamini Keane ataendelea kuimarika.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: EVERTON YASAJILI BEKI LA MAN UNITED PAUNI MILIONI 30 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top