• HABARI MPYA

    Thursday, July 13, 2017

    AVEVA, KABURU MAMBO MAGUMU…WARUDISHWA RUMANDE HADI JULAI 20

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KESI inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Elieza Aveva na Makamu wake, Geofrey Hiriki Nyange ‘Kaburu’, imeahirishwa hadi Julai 20, mwaka huu na watuhumiwa hao wamerudishwa rumande.
    Kesi hiyo imetajwa tena leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Victoria Nongwa baada ya watuhumiwa hao kusomewa mashtaka yao kwa mara ya kwanza Juni 29, mwaka huu.
    Viongozi hao wanakabiliwa na makosa matano wanayodaiwa kuyafanya kwa nyakati tofauti yakiwemo ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana.
    Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili ni pamoja na kughushi nyaraka zinazodaiwa kuwa klabu ya Simba inawalipa madeni watuhumiwa hao kiasi cha dola za Kimarekani 300,000 (Zaidi ya shilingi milioni 700 za kitanzania).
    Makosa mengine ni Aveva kutoa nyaraka za uongo kwa Benki ya CRDB Tawi la Azikiwe Dar es Salaam Machi 10, 2016, la tatu ni kutakatisha fedha kinyume cha sheria, ambapo inadaiwa rais huyo na Kaburu walikula njama za kufanya uhalifu huo.
    Shtaka la nne ni Kaburu kutakatisha fedha dola 300,000 na kuziweka katika Benki ya  Barclays Tawi la Mikocheni mjini Dar es Salaam, na la tano ni kutakatisha fedha  likimhusu tena, Makamu wa Rais, Kaburu anayedaiwa kumsadia Aveva kutakatisha fedha katika benki ya Barclays baada ya kughushi nyaraka.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AVEVA, KABURU MAMBO MAGUMU…WARUDISHWA RUMANDE HADI JULAI 20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top