• HABARI MPYA

    Friday, May 03, 2013

    VILLA BOAS AWAKATA MAINI REAL MADRID NA ZIDANE; AWAAMBIA GARETH BALE HANG'OKI SPURS HATA KWA PAUNI MILIONI 60

    KOCHA Andre Villas-Boas hana shaka Gareth Bale ataendelea kuwa mchezaji wa Tottenham msimu ujao, akisema kwamba hata itolewe ofa ya Pauni Milioni 60 hatamuuza.
    Nyota huyo wa Wales, ambaye leo ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Kandanda England, amekuwa katika msimu mzuri, akitoa mchango mkubwa kwa Spurs.
    Akiwa amefunga mabao 19 katika mechi 29 za Ligi Kuu England, Bale ameendelea kuzikuna klabu kubwa, zikiwemo Real Madrid na Bayern Munich ambazo zinaitaka saini yake kwa gharama yoyote.
    Hot Spur: Gareth Bale brilliance all season has kept Tottenham in the hunt for a top four place
    Hot Spur: Gareth Bale brilliance all season has kept Tottenham in the hunt for a top four place
    Hot Spur: Gareth Bale brilliance all season has kept Tottenham in the hunt for a top four place
    Gwiji la Ufaransa, Zinedine Zidane, ambaye anafanya kazi kama Mshauri Maalum wa vigogo wa Hispania, Real amesema jana kwamba kiasi cha Pauni Milioni 48, ambazo Madrid waliliipa Juventus kumpata yeye zaidi ya muongo uliopita, kupata saini ya winga huyo.
    Pamoja na hayo, Villas-Boas amejibu leo, akisema: "Hata kama kiwango hicho cha fedha kinamlenga mchezaji huyo, haijalishi kwetu, kwa sababu ni mchezaji wetu na mchezaji ambaye tunatakiwa kuendelea kuwa naye kuhakikisha tunatimiza malengo yetu na kuendeleza harakati. 
    "Taarifa nilizonazo kutoka kwenye klabu klabu ni kwamba, mchezaji huyo yupo hapa kubaki, hata ikiwa tutapata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa au la. Klabu lazima iendelee mbele kwa kuwashikilia wachezaji wazuri,".
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: VILLA BOAS AWAKATA MAINI REAL MADRID NA ZIDANE; AWAAMBIA GARETH BALE HANG'OKI SPURS HATA KWA PAUNI MILIONI 60 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top