• HABARI MPYA

    Thursday, May 09, 2013

    SIMBA SPORTS CLUB YAANDAA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN)


    Simba Sports Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafaamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (strategic plan).
    Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-

    1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
    2. Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
    3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.

    Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013   Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-

    1. Joseph Itang’are
    2. Swedy Mkwabi
    3. Francis Waya
    4. Ramesh Patel
    5. Evance Aveva
    6. Mulamu Ng’hambi
    7. Salim Mhene
    8. Mtemi Ramadhani
    9. Moses Basena
    10. Henry Tandau
    11. Omary Gumbo
    12. Michael Wambura
    13. Glory Nghayomah
    14. Crensencius Magori
    15. Honest Njau
    16. Ruge Mtahaba
    17. Evodius Mtawala
    18. Dr Mwafyenga

    Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
    Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.
    Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.
    Mpango mkakati huo utakuwa tiyari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.

    Imetolewa na 
    Evodius Mtawala
    Katibu Mkuu,
    Simba Sports Club. 
    9/5/2013
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SPORTS CLUB YAANDAA MPANGO MKAKATI (STRATEGIC PLAN) Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top