• HABARI MPYA

    Thursday, May 09, 2013

    NYOTA WANNE SIMBA SC WAENDA UJERUMANI

    Simba SC ya yosso

    Na Prince Akbar, IMEWEKWA MEI 9, 2013 SAA 12:28 JIONI
    WACHEZAJI wanne chipukizi wa klabu ya Simba SC, Emilly Mgeta, Sadi Ndemla, Miraji Madenge na Frank Sekule wameondoka jana nchini kwenda Ujerumani kwa ajili ya kambi maalum ya soka, inayohusisha vijana wengine mbalimbali duniani.
    Katibu wa Simba SC, Evodius Mtawala ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, nyota hao wanne wa Simba wameondoka kwa pamoja na vijana wengine wa Kitanzania.
    Mtawala alisema wakiwa huko, watakuwa katika kambi maalum ya soka, ambako watapata fursa ya kutazamwa na mawakala mbalimbali na kama wataonyesha uwezo wa kuridhisha wanaweza kupata timu.
    “Kuna wakala Mtanzania kawachukua kawapeleka huko, ametuambia katika hiyo kambi kama wachezaji wetu wataonyesha uwezo, ambao utawavutia mawakala, basi Simba SC inaweza kupata nafasi ya kuwauza,”alisema Mtawala.
    Mtawala alisema kwamba sera ya Simba SC si kuwabana wachezaji wanapopata nafasi na ndiyo maana imewaruhusu ‘makinda’ hao wakajaribu bahati yao.
    “Sisi tuna mtazamo wa kimaendeleo sana, na ndiyo maana ukitazama katika nchi hii, sisi ndiyo ambao kama klabu tumetoa idadi kubwa ya wachezaji waliocheza, na wanaocheza nje,”alisema Mtawala.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: NYOTA WANNE SIMBA SC WAENDA UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top