• HABARI MPYA

    Friday, May 03, 2013

    MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC LEO MOROCCO KABLA YA KUVAANA NA AS FAR RABAT KESHO PRINCE MOULAY ABDELLAH

    Kiungo tegemeo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy Jr.' akipiga mpira pembeni ya kiungo mwenzake, Khamis Mcha 'Vialli' wakati wa mazoezi wa timu hiyo jioni ya leo kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat ambao utatumika kwa mchezo wa kesho wa marudiano, Raundi ya Tatu Kombe la Shirikisho Afrika, dhidi ya wenyeji AS FAR Rabat kuanzia saa 11:00 kwa saa za huku na saa 1:00 usiku kwa saa za Tanzania.

    Pamoja na baridi kali la huku, lakini kutokana na mazoezi makali, Joh Bocco 'Adebayor' anapoza koo

    Malika Ndeule anapiga mpira kumpasia Kipre Tchetche dhidi ya Gaudence Mwaikimba kushoto

    Meneja Msaidizi, Jemedari Said akipiga danadana kukumbushia enzi zake Uwanja wa Ilulu, Lindi akiichezea Kariakoo United.

    Makipa wa Azam na kocha wao, Iddi Abubakar mwenye jezi nyeupe wakiomba dua kabla ya kuanza mazoezi

    Kuusaka upepo; Wachezaji wa Azam wakikimbia kuuznguka Uwanja wa Prince Moulay Abdellah

    Sure Boy Jr. akijiandaa kuanza mazoezi

    Waingereza; Kocha Mkuu, Stewart Hall akijadiliana jambo na Msaidizi wake, Kali Ongala kabla ya kuanza mazoezi

    Kipre Tchetche na Himi Mao nyuma ndani ya basi wakitokea mazoezini

    Brian Umony kulia na Humphrey Mieno kushoto ndani ya basi

    Basi limefika Golden Tulip, hoeli ambayo imefikia Azam

    David Mwantika kulia akipiga mpira pembeni ya Kipre Balou

    Nje ya hoteli ya Giolden Tulip...

    Hayakuwa mazoezi ya kitoto...

    Wa nani huo? Seif Abdallah kulia, Mieno kushoto na Abdi Kassim 'Babbi' katikati

    Khamis Mcha 'Vialli'

    Kipa Mwadini Ally akidaka mpira wa juu

    John Bocco 'Adebayor' kulia akimiliki  mpira pembeni ya Luckson Kakolaki

    Jabir Aziz akimiliki mpira pembeni ya John Bocco

    Daktari Mwanandi Mwankemwa kushoto akimtazama John Bocco baada ya kuumia goti. Kulia Kali Ongala na nyuma ni Sure Boy. Hata hivyo, Bocco hakupata maumivu makali, aliinuka na kuendelea na mazoezi. Lakini ni goti lile lile ambalo huwa linamuweka nje ya Uwanja mara kwa mara.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC LEO MOROCCO KABLA YA KUVAANA NA AS FAR RABAT KESHO PRINCE MOULAY ABDELLAH Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top