• HABARI MPYA

    Saturday, May 04, 2013

    MANCINI AKALIA KUTI KAVU MAN CITY, UONGOZI WAKUTANA NA WAKALA WA PELLEGRINI MADRID


    KOCHA Roberto Mancini anakabiliwa na wakati mgumu Manchester City baada ya kusema kwamba amepata taarifa za klabu hiyo kukutana na wakala wa Manuel Pellegrini.
    Pellegrini anatajwa kama mmoja wa walimu wenye nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake mwishoni mwa msimu na Mancini anatarajia kupewa ufafanuzi kutka kwa mabosi wa City baada ya Mkurugenzi wa Soka, Txiki Begiristain kukutana na mwakilishi wa kocha huyo wa Malaga kwa chakula cha jioni mjini Madrid.
    Alipoulizwa kama Mwenyekiti, Khaldoon Al Mubarak alimuambia kama atabaki kazini, kocha huyo wa City alisema: "Hajawahi, hajawahi. Hatuna haja ya kulizungumzia hili. Hatuna matatizo yoyote. Tuna uhusiano mzuri. Katika miaka miwili, tumeshinda mataji matatu, na sasa tuna nafasi ya kushinda taji lingine moja,"alisema. 
    Centre of attention: Roberto Mancini admits he is in the dark over his Manchester City future
    Katikati ya lolote: Roberto Mancini amesema mustakabali wake upo kizani Manchester City
    Second best: Manchester City failed to retain the Premier League title this season
    Wa pili bora: Manchester City imeshindwa kutetea taji la Ligi Kuu msimu huu

    'Ikiwa katika miaka mitatu nisingeshinda taji, hapo sawa, lakini tumefanya kazi nzuri hadi sasa. Tuna nafasi ya kutwaa Kombe la FA na kuwa wa pili katika msimamo wa Ligi Kuu. Baada ya hapo, Mwenyekiti anaweza kuchukua uamuzi wowote kuhusu kocha, Hatuna tatizo lolote. Nimechanganyikiwa, kwa sababu nataka kushinda taji la pili la Ligi Kuu. Tulikuwa na nafasi, lakini wakati mwingine unaweza kufanya makosa. 
    "Unaweza kumuuliza maswali hayo Txiki, lakini si muhimu kwangu. Nafikiri alikuwa ana chakula kizuri cha jioni.
    MANUEL PELLEGRINI
    Txiki Begiristain
    Majadiliano: Txiki Begiristain (kulia) alifanya mazungumzo na wakala wa Manuel Pellegrini wakati wa chakula cha jioni 
    Target: Former Chelsea manager Jose Mourinho has been linked with a move to the Etihad Stadium
    Anatakiwa: Kocha wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho amekuwa akihusishwa pia na kuhamia Etihad 

    "Kwa miezi sita iliyopita, watu wameandika kila kitu, walianza na Pep Guardiola na Jose Mourinho, kisha Pellegrini, Carlo Ancelotti na Brendan Rodgers. Najua nafanya kazi na watu makini, kama Khaldoon na Sheikh Mansour, lakini kama kulikuwa kuna kocha mwingine aliyeshinda mataji matatu ndani ya miaka miwili, usingesema kitu juu yake." 
    Mancini tayari ameanza mikakati ya msimu ujao na angependa kuongeza mshambuliaji, beki wa kati, kiungo mkabaji, mchezeshaji na winga. 
    Lakini kutokana na kuingia kwenye uhusiano mbaya na baadhi ya wachezaji waandamizi mustakabali wake uko kwenye hatihati.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MANCINI AKALIA KUTI KAVU MAN CITY, UONGOZI WAKUTANA NA WAKALA WA PELLEGRINI MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top