• HABARI MPYA

    Thursday, May 02, 2013

    ALONSO MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA


    KOCHA Jose Mourinho yuko tayari kumfanya Xabi Alonso awe mchezaji wa kwanza kusajiliwa atakaporejea Stamford Bridge mwishoni mwa msimu kuifundisha tena Chelsea.
    Kocha huyo wa Real Madrid alihusishwa kwa kiasi kikubwa na kurejea Chelsea baada ya timu yake kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Ulaya akihama Bernabeu mwishoni mwa msimu.
    Kocha huyo wa Kireno mwenye umri wa miaka 50 alisema atakwenda sehemu ambayo anapendwa, vyombo vingi vya habari vikisema Magharibi mwa London, ambako aliifundisha Chelsea akiibebesha mataji matatu kabla ya kuondoka mwaka 2007 ndiko anakopendwa zaidi.
    This way to Chelsea: Jose Mourinho could bring Xabi Alonso with him to London
    Huku kuelekea Chelsea: Jose Mourinho atahamia na Xabi Alonso na London
    Joining Jose? Alonso (right) is believed to be on Mourinho's wishlist, should he take charge of Chelsea this summer
    Unaondoka Jose? Alonso (kulia) inaaminika yuko kwenye mipango ya Mourinho, akihamia Chelsea mwishoni mwa msimu
    Inafahamika kwamba Mourinho tayari amemtambulisha nyota huyo wa zamani wa Liverpool kama mmoja wa wachezaji atakaowasajili ikiwa atakwedna kurithi mikoba ya Rafa Benitez.
    Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 wa kimataifa wa Hispania, ambaye alitwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Liverpool mwaka 2005, atamaliza mkataba wake msimu ujao na bado hajakubali ofa ya nyongeza ya mkataba wa miaka kuendelea kuishi Madrid.
    Kwa mujibu wa gazeti la Independent, Alonso ni mmoja kati ya marafiki wa karibu wa Mourinho ndani ya Real na amesitisha uamuzi wake hadi ajue nani atarithi mikoba ya Mreno huyo.
    Akihamia Chelsea, dhahiri atawaumiza mashabiki wa Liverpool, kwani aliwahi kusema atakaribisha ofa ya kurejea Anfield.
    Wazi pia akihamia Stamford Bridge itakuwa utata kati yake na kiungo wa England, ambaye pia ni swahiba wa Mourinho, Frank Lampard aliyekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja.
    Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Rademel Falcao, waakti huo huo inaaminika ni mchezaji anayetakiwa zaidi The Blues, ingawa kuna mchuano mkali na klabu nyingine, Manchester United na Manchester City kuwania saini ya Mcolombia huyo.

    VITA KATIKA KIUNGO - ALONSO v LAMPARD

    Hold up: Frank Lampard could complicate a move for former Liverpool favourite Alonso to join Chelsea, should he agree a new one-year contract extension
    Pishaa: Frank Lampard ataingia kwenye mchuano wa namba na nyota wa zamani wa Liverpool, Alonso akijiunga na Chelsea, akikubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja
    Early bath, Frank: Lampard was sent off for this challenge on Xabi Alonso in 2009
    Enzi hizo, Frank: Lampard alitolewa kwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Xabi Alonso mwaka 2009
    Getting stuck in: Lampard slides in on Alonso in 2005
    Anampa kitu: Lampard akiteleza kwenye miguu ya Alonso mwaka 2005
    Tussle at the top: Lampard (right) and Alonso go for the ball during a Champions League semi-final
    Jino kwa jino: Lampard (kulia) na Alonso wakigombea mpira katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: ALONSO MCHEZAJI WA KWANZA KUSAJILIWA NA MOURINHO CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top