• HABARI MPYA

    Friday, May 03, 2013

    25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS

    Seif Abdallah kushoto. Yupo na Azam Rabat.

    Na Boniface Wambura
    WACHEZAJI 25 kati ya 30 walioitwa na Kocha Kim Poulsen kwenye kikosi cha pili cha Taifa Stars (Young Taifa Stars) wameripoti kambini ambapo mazoezi yalianza tangu jana jioni (Mei 2 mwaka huu).
    Kocha Kim amewaita wachezaji hao katika kambi hiyo ya siku tano ili kuangalia uwezo wao katika maeneo kadhaa kwa lengo la kupata baadhi ambao anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars siku za usoni.
    Wachezaji watano walioshindwa kujiunga katika kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Sapphire jijini Dar es Salaam ni Aishi Manula, David Mwantika, Himid Mao, Samih Nuhu na Seif Abdallah ambao wako Morocco na timu yao ya Azam.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: 25 WARIPOTI KAMBINI YOUNG TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top