• HABARI MPYA

    Friday, February 08, 2013

    PITROIPA WA BURKINA FASO RUKSA KUCHEZA FAINALI JUMAPILI BAADA YA REFA JDIDI KUKIRI ALIMUONEA KUMPA NYEKUNDU DHIDI YA GHANA


    Jonathan Pitroipa na refa Jdidi

    MSHAMBULIAJI nyota wa Burkina Faso, Jonathan Pitroipa, ambaye alilimwa kadi nyekundu katika Nusu Fainali Jumatano anajiandaa kucheza Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Jumapili dhidi ya Nigeria.

    Hadi Pitroipa kuwa tayari kucheza mechi ya Jumapili, ilibidi refa wa Jumatano kati ya Burkina Faso na Ghana, Slim Jdidi wa Tunisia akiri alifanya makosa kumpa kadi ya pili ya njano mchezaji huyo kwa kujirusha, amesema rais wa CAF, Issa Hayatou.
    "Kila mtu anasema huyu refa hakuchezesha vizuri hii mechi," alisema Hayatou leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: PITROIPA WA BURKINA FASO RUKSA KUCHEZA FAINALI JUMAPILI BAADA YA REFA JDIDI KUKIRI ALIMUONEA KUMPA NYEKUNDU DHIDI YA GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top