• HABARI MPYA

    Saturday, February 09, 2013

    MBUYU, KIIZA, NIYONZIMA WAREJEA YANGA BAADA YA MAJUKUMU YA KITAIFA



    Haruna Niyonzima (kulia) akiongea na Godfrey Taita wakati wa mazoezi CCM Kirumba
    Wachezaji wa kimataifa wa timu ya Young Africans Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite (Rwanda) na Hamis Kiiza (Uganda) wanatarajiwa kuwasili leo jioni tayari kwa kuungana na wachezaji wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Africa Lyon siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
    Kuwasili kwa wachezaji hao watatu ambao walikwenda kuzitumikia timu zao za Taifa katika michezo ya kirafiki iliyofanyika katikati ya wiki, kutakifanya kikosi cha Young Africans kukamilika wachezaji wote kufuatia wachezaji waliokuwa timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) kuanza mazoezi jana.
    Young Africans itakua na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumatano dhidi ya timu inayoshika mkia ya African Lyon mchezo ambao utakua mzuri kwani African Lyon watataka kupata ushindi ili waweze sogea katika nafasi ya mwisho kwenye msimamo huku Yanga nayo ikihitaji point 3 ili iweze kuendelea kukaa kileleni.
    Kocha Mkuu Ernest Brandts mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi katika uwanja wa mabatini Kijitonyama ametoa mapumziko ya siku mbili  kwa wachezaji  hivyo kesho jumamosi na keshokutwa jumapili hakutakua na mazoezi na timu itaingia kambini siku ya jumapili jioni kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
    Aidha Brandts amesema watahakikisha wanacheza vizuri na kuibuka na ushindi katika mchezo wa jumatano ili kuendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom hatua itakayopelekea pia kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa Ubingwa.
    Katika kikosi kilichoendelea na mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa mabatini hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja na wachezaji wote wako fit tayari kabisa kwa mpambano huo dhidi ya African Lyon
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: MBUYU, KIIZA, NIYONZIMA WAREJEA YANGA BAADA YA MAJUKUMU YA KITAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top