• HABARI MPYA

    Sunday, February 10, 2013

    BARCLAYS YAPELETA WATEJA KUSHUHUDIA FAINALI AFCON

    Mrembo shabiki wa Nigeria

    Na Prince Akbar
    BENKI ya Barclays Tanzania imepeleka wateja wake kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) inayochezwa leo mjini Johannesburg, Afrika Kusini.
    Mkuu wa kitengo cha Mawasilino na Mahusiano  wa Barclays Tanzania, Tunu Towo Kavishe amesema Barclays imeona kuwa ni vema kupeleka baadhi ya wateja wake kushuhudia pambano hilo kwa macho yao kwa gharama za benki hiyo.
    “Tumefikia uamuzi huu wa kupeleka baadhi ya wateja wetu kushuhudia fainali hiyo kutokana na kutambua mchango wao mkubwa katika maendeleo ya benki yetu, nah ii ni alama au ishara ya shukrani zetu kwao,” anasema bi. Tunu.
    Bi Tunu akaongeza kusema kuwa Barclays Tanzania inafahamu umuhimu wa wateja wao pamoja na jamii kwa ujumla katika kujishirikisha kwenye michezo na burudani kwa ajili ya kuimarisha afya ya mwili na akili, kitu ambacho ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa shughuli zao za kila siku, na ni imani ya Barclays Tanzania kuwa wateja waliopata nafasi hiyo watapata burudani ya aina yake kwa kuwashuhudia miamba wawili wa Afrika waliotinga fainali, Super Eagles ya Nigeria na Burkina Faso.
    Hii si mara ya kwanza kwa Barclays Tanzania kupeleka wateja wake nje ya nchi kushuhudia mechi za soka za kimataifa kwani miaka michache iliyopita, benki hii kongwe zaidi nchini iliendesha promosheni ya Barclays Premier League (BPL) na kuwapeleka Watanzania kadhaa kushuhudia mechi za Ligi Kuu ya England inayofadhiliwa na benki hiyo.
    Kwa kupitia promosheni hiyo, mteja mmoja na mwenza wake walishinda tiketi ya safari ya kwenda Uingereza na kurudi huku pia wakishuhudia moja ya mechi za ligi hiyo maarufu zaidi duniani kwa gharama ya Barclays.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: BARCLAYS YAPELETA WATEJA KUSHUHUDIA FAINALI AFCON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top