• HABARI MPYA

  Jumanne, Mei 29, 2012

  RIHANNA KATIKA PENZI JIPYA SHATASHATA


  Rihanna and J.R. Smith
  Wapenzi... Rihanna na J.R. Smith
  Published: 42 minutes ago

  RIHANNA ameibuka tena katika uga wa mahaba, safari hii tetesi zikisema anamoa uroda nyota wa mpira wa kikapu, J.R. Smith.

  Mwimbaji huyo nyota amekuwa akihusishwa na mcheza kikapu mwenye ma-tatoo kibao, tangu wakutwe pamoja wakijirusha katika  klabu ya usiku, New York mwezi huu.
  Na Rihanna ameendelea kuzipa uzito tetesi hizo baada ya Jumapili kusimama mkali huyo wa New York Knicks mjini Miami.
  Wawili hao walijirusha hadi 'majogoo' katika klabu la LIV kwenye hoteli ya Fontainebleau, ambako bwana wa zamani wa Rihanna, Drake alionekana akizubaa, kwa mujibu wa gazeti la kila siku la New York Daily News.
  Smith anaonekana ni bwana mwingine 'mtukutu' aliyempata Rihanna.
  Alichukuliwa kwenye benchi Alhamisi kwa kosa la kuendesha gari na leseni ambayo si stahili, kabla ya kuachiwa Ijumaa.
  Pia hivi karibuni alitozwa faini ya pauni 16,000 na NBA baada ya kubandika picha ya kumdhalilisha mwanamke kwenye tweeter.
  Lakini bado ana mwonekano wa kuweza kumridhisha kimwana huyo kitandani.
  Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alikiri anaimba kuhusu mapenzi kwa sababu anahisi haridhishwi kwenye ngono.
  Hivi karibuni alihusishwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na bondia Muingereza, Dudley O’Shaughnessy, mwenye umri wa miaka 22, ambaye alicheza katika video yake ya We Found Love.
  Rihanna and Chris Brown
  Wapenzi wa zamani... Rihanna na Chris Brown
  Alikuwa akifuatiliwa kwa karibu na nyota wa Ashton Kutcher, mwenye umri wa miaka 34 — ambaye alijirusha naye hadi saa 10 alfajiri, Machi, mwaka huu.
  Mahusiano ya muda mrefu ya kimapenzi ya nyota huyo yalikuwa na mwimbaji mwenzake, Chris Brown, lakini waliachana wakati alipopigwa na mwanaume huyo mwaka 2009
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RIHANNA KATIKA PENZI JIPYA SHATASHATA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top