• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 26, 2012

  MALAWI, STARS ZATOSHANA NGUVU

  TIMU za soka za taifa zaTanzania, Taifa Stars na Malawi ‘The Flames’ leo zimeshindwa kutambiana baada ya kulazimisha sare ya 0-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
  Mchezo huo ulikuwa ni mahususi kwa timu hizo kujinoa kwa ajili ya mechi zake za mchujo wa kuwania kucheza Kombe la Dunia Juni 2, ambapo Stars itakuwa Ivory Coast, huku Malawi itakwaana na Kenya ambapo zote zitacheza ugenini.
  Mpaka mwamuzi wa mchezo huo Oden Mbaga anapuliza filimbi ya mwisho, hakuna rimu iliyofanikiwa kutikisa nyavu za mwezake.
  Stars:Juma Kaseja, Shomari Kapombe, Wazir Salum/Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondan, Shaban Nditi, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samatta, Haruna Moshi ‘Boban’na Mwinyi Kazimoto.
  Malawi:Simplex Nthala, Limbikani Mzava, Moses Mvula, Foster Namwela, James Sangala, Joseph Kamwendo, Frank Banda, Dave Banda/Jimmy Zakazaka, Zicco Mkanda/Amadu Ally, Robin Ngalande na Russell Mwafulirwa/ Ndaziona Chatsalira.

  Wachezaji wa Taifa Stars wakitoka uwanjani baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza
  Mbwana Samatta wa Taifa Stars akijaribu kumtoka beki wa Malawi, Foster Namwela.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALAWI, STARS ZATOSHANA NGUVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top