• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 27, 2012

  BECKHAM APUNGUZIWA MSHAHARA GALAXY, SAA APIGWA BAO NA THIERRY HENRY


  Pato lake lapungua kwa asilimia 40

  Lakini bado anatengeneza pauni Milioni 29 kwa mwaka

  Published: Today at 00:19

  MWANASOKA nyota, David Beckham amepunguziwa mshahara kwa zaidi ya dola za Kimarekani Milioni mbili — ambayo ni sawa na kushuka kwa asilimia 40 ya pato lake.

  Inamaanisha nyota huyo wa LA Galaxy ameondoka kwenye orodha ya wanasoka wanaolipwa fedha nyingi katika Ligi ya Marekani, akina Thierry Henry, ambaye anachezea New York Red Bulls.
  Becks, mwenye umri wa miaka 37, amekuwa akilipwa zaidi ya pauni Milioni 4 (dola Milioni 6.5) kwa mwaka.
  Lakini amekubali kulipwa pauni Milioni 2.5, baada ya kuamua kubaki California na mkewe Victoria, mwenye umri wa miaka 38, na watoto wao wanne.
  Pamoja na hayo, anapata makato ya mauzo ya tiketi za Galaxy na vifaa vya michezo. Na ataendelea kupata kiasi cha jumla ya pauni Milioni 29 kwa mwaka, kupitia dili za mauzo ya nguo maslahi ya kibiashara, kwa mujivu wa orodha ya wanamichezo matajiri ya jarida la Forbes.
  Nahodha huyo wa zamani wa England, Becks angeweza kujiingizia fedha nyingi zaidi kama angekubali kuhamia Paris Saint-Germain. 
  Chart showing what David Beckham is worth
  Mapato ya Becks...
  Becks anayeshika nafasi ya 32 katika orodha ya watu maarufu matajiri 100 ya jarida la Forbes, imeelzwa: “Ni kama utakuwa mkataba wa mwisho kama kwa Beckham wakati akielekea mwishoni mwa miaka yake ya 30. Haonyeshi dalili za kushuka kiwango uwanjani.
  David and Victoria Beckham's new summer house in Malibu
  Mjengo mpya Beckham uliopo mjini Malibu
  EROTEME.CO.UK
  Henry, mwenye umri wa miaka 34, ana mkata wa pauni milioni 3.1, wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Ireland, anayechezea Galaxy pia, Robbie Keane, mwenye umri wa miaka 31, anashika nafasi ya nne kwa kulipwa pauni Milioni 2 kwa mwaka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BECKHAM APUNGUZIWA MSHAHARA GALAXY, SAA APIGWA BAO NA THIERRY HENRY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top