• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 28, 2012

  MILIONEA WA YANGA ANENA BUSARA TUPU


  Bin Kleb akimkabidhi jezi Haruna Niyonzima baada ya kumsajili mwaka jana mjini Kigali 'kwa bei chafu' kutoka APR ya Rwanda

  MDAU wa soka nchini, Abdallah Ahmed Bin Kleb ameomba ijitokeze kampuni ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, ili kuwawezesha kujimudu na kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY usiku huu, Bin Kleb aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, kabla ya kujiuzulu alisema kwamba marefa wa Tanzania wanafanya kazi katika mazingira magumu na wanalipwa posho kidogo mno na TFF.
  “Nasikia wanalipwa Sh. 70,000, hizi ni fedha kidogo sana, haziwezi kuwatosheleza kujikimu, naomba ijitokeza kampuni maalum, kwa ajili ya kuwadhamini marefa wa Ligi Kuu, kwa sababu kwa kufanya hivyo kampuni zitanufaika kwa sababu watatangazwa kibiashara,”alisema.
  Bin Kleb alisema kwamba, wakati mwingine watu wanakosea kuwatupia shutuma nyingi waamuzi kwamba wanapenda rushwa, ingawa hutokea hatakwa  waamuzi walio waadilifu wakaingia kwenye mitego kwa sababu ya hali halisi inayowakabili.
  Aidha, Bin Kleb alisema anastaajabishwa mno na vyombo vya habari nchini, kuelekeza nguvu zao katika mechi za Ligi Kuu zinazochezwa Dar es Salaam pekee, wakati mikoani ndiko kuna mambo mengi ‘ya ajabu’.
  “Unakuta Televisheni zinaonyesha mechi za Dar es Salaam pekee, wakati huko mikoani ndiko kuna mambo ya ajabu kweli kweli, ambayo yanatakiwa yaripotiwe ili yakomeshwe, kwa hivyo natoa haya mawili kama changamoto kwa maslahi ya soka yetu,”alisema Bin Kleb.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MILIONEA WA YANGA ANENA BUSARA TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top