• HABARI MPYA

  Jumatatu, Mei 28, 2012

  CECH ASAINI MKATABA MPYA CHELSEA MIAKA MINNE  EPL:Petr Cech, Chelsea v Newcastle United
  Cech  KIPA wa ChelseaPetr Cech amemwaga wino akitia saini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu hiyo bingwa Ulaya kwa miaka minne zaidi.
  Kipa huyo wa kimataifa wa Czech, alijiunga na The Blues mwaka 2004, akitokea Rennes Ufaransa kwa dau la pauni Milioni 9 na hadi sasa amedaka mechi 369 katika klabu hiyo, akiiwezesha kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu ya England, manne ya FA, mawili ya Carling na moja la Ligi ya Mabingwa na s
  asa atakuwa Stamford Bridge hadi mwaka 2016.


  "Ninafurahi mno kuwa ni sehemu ya klabu hii maarufu kwa kipindi cha miaka mine zaidi," alielezea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30.
  "Ninatumaini miaka hiyo minne ijayo itakuwa ni sawa na miaka minane ambayo nimekuwa nikikichezea klabu."
  Cech, ambaye mkataba wake wa awali ulikuwa umalizike mwaka ujao, ni mchezaji muhimu kwa Chelsea
  Cech pia alitangazwa kama mchezaji bora zaidi wa Chelsea mwaka jana, 2010/11.
  "Chelsea inatambua kikamilifu mchango muhimu kutoka kwa Petr wakati huu wa klabu kupata ufanisi wake mkubwa zaidi katika historia yake," alielezea mkurugenzi mkuu wa Chelsea, Ron Gourlay.
  Kipa msaidizi wa Cech, Thibaut Courtois kutoka Ubelgiji, huenda akaachiwa mechi zaidi za ligi kuu ya Premier ili kujinoa zaidi, baada ya kuonyesha uhodari wake akiwa mchezaji wa mkopo katika klabu ya Uhispania ya Atletico Madrid, ijapokuwa kijana huyo wa miaka 20 huenda akaazimwa kwa timu nyingine kwa muda mfupi.
  Courtois alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Racing Genk, mwezi Julai mwaka jana, na kwa kuelekea Uhispania na kutofungwa, aliiwezesha klabu ya Atletico Madrid kuibuka mabingwa wa klabu ya Europa mapema mwezi huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CECH ASAINI MKATABA MPYA CHELSEA MIAKA MINNE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top