• HABARI MPYA

    Sunday, May 27, 2012

    TIMU YA MATOLA YAIFUATA AZAM


    SuperSport beat Sundowns to win Cup
    KLABU ya SuperSport United ya Afrika Kusini jana iliwafunga Mamelodi Sundowns waliomaliza mechi wakiwa pungufu ya mchezaji mmoja, mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Orlando na kutwaa Kombe la FA la Afrika Kusini kwa mara ya tatu. 
    Beki wa kati wa Sundowns Clayton Daniels alitolew3a nje kwa kadi nyekundu dakika ya 19, baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa SuperSport, Kermit Erasmus kwejnye eneo la penalti.
    Mbali na hundi ya dola za Kimarekani 720,000, kwa kutwaa taji hilo, SuperSport timu aliyowahi kuchezea kiungo wa zamani wa Simba SC, Suleiman Matola imejikatia tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho la Soka Afrika mwakani, michuano ambayo kwa Tanzania, mwakilishi wake ni Azam FC.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU YA MATOLA YAIFUATA AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top