• HABARI MPYA

  Jumamosi, Mei 26, 2012

  MBRAZIL WA UKWELI AOMBA KAZI YANGA

  ALIYEWAHI kuwa kocha Msaidizi wa timu ya soka ya taifa ta Tanzania, Taifa Stars, Mbrazil Itamar Amorin ni miongoni mwa makocha 20 wanaowania  kuifundiha klabu bingwa ya zamani nchini, Yanga.
  Itamar alikuwa Msaidizi wea Marcio Maximo katika kikosi cha Taifa Stars kabla ya kuacha kazi na kurejea kwao.
  itamar, ambaye baada ya kuachana na Stars alirejea nchini kufundisha Azam FC, yupo kwenye orodha ya makocha wanaowania kurithi mikoba ya Mserbia, Kostadin Bozidar  Papic Yanga.
  IKatibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa ameaiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba makocha wengine walioomba kazi Jangwani ni raia wa Ureno, England, Uhoianzi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ufaransa, Afrika Kusini na Australia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBRAZIL WA UKWELI AOMBA KAZI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top