ETI wanachama 700 wa Yanga walikutana Jumapili makao makuu
ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam na kufikia uamuzi
wa kumng’oa madarakani Mwenyekiti, Wakili Lloyd Bahargu Nchunga.
Mapinduzi haya yaliongozwa na Mzee Ibrahim Akilimali, ambaye
kihistoria nilishasema siku nyingi ni mzee kinara wa migogoro na mvuruga amani
klabuni.
Kweli, Nchunga ameshindwa kuongoza Yanga na sababu kubwa ni
uelewa wake mdogo katika masuala ya michezo na kukosa ushirikiano kutoka kwa
Wajumbe wenzake wa Kamati ya Utendaji na wadau wengine wa klabu, wakiwemo hao
wanaojiita wazee.
Lakini ukirejea uchaguzi uliomuweka madarakani Nchunga Jumapili
ya Mei 18, mwaka 2010, alishinda Uenyekiti baada ya kupata kura 1,437, akiwaangusha wapinzani wake wanne, Francis
Kifukwe aliyepata kura 370, Mbaraka Igangula aliyepata kura 305, Abeid Falcon
aliyepata kura 301 na Edgar Chibura aliyeambulia kura 65 katika kura 2,220
zilizopigwa, wakati kura 23 kati ya hizo ziliharibika.
Kura 370 za Kifukwe na 305 za Igangula kwa pamoja
wakichanganya, bado hawawezi kufikia kura za Nchunga- ina maana alishinda kwa
kishindo. Inakuwa rahisi kuhisi watu hawa 700 waliokutana Jumapili ni wale wale
700 waliomnyima kura Nchunga PTA Mei 18, 2010.
Sitaki kuzama ndani sana- kwa sababu nimeshapitisha sera ya
kutoandika habari za migogoro- lakini kwa pamoja na wasomaji wangu napenda tujadili,
kiongozi aliyeshinda kwa kura 1,437 anaweza kung’olewa madarakani na watu 700?
Tena watu ambao
hakuna aliyewahakiki kama kweli ni 700 na hakuna aliyehakikisha kama kweli ni
wanachama wa Yanga? Tujadili.
LLOYD NCHUNGA
MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI YA YANGA, RIDHIWAN KIKWETE AKITANGAZA MATOKEO MEI 19, 2010, KULIA NI MFADHILI WA KLABU HIYO, YUSUF MANJI
MAKAMU MWENYEKITI, DAVIS MOSHA AKITOA SHUKURANI KWA WANACHAMA
SARAH RAMADHAN ALIYESHINDA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI
ALLY MAYAI TEMBELE ALIYESHINDA UJUMBE
CHARLES MUGONDO ALIYESHINDA UJUMBE
THEOFRID RUTASHOBORWA (SASA MAREHEMU) ALIYESHINDA UJUMBE
SALIM RUPIA ALIYESHINDA UJUMBE
MZEE YUSSUF ALIYESHINDA UJUMBE
MOHAMMED BHINDA ALIYESHINDA UJUMBE
0 comments:
Post a Comment