• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 27, 2012

  KASEJA AANGUA KILIO DAR LIVE


  Kaseja akilia, akibembelezwa na Machaku

  KIPA wa Simba, Juma Kaseja jioni hii ameshindwa kujizuia lilipotajwa jina la Patrick Mafisango kwenye sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya klabu hiyo na kujikuta akimwaga machozi kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala, Dar es Salaam.
  Kaseja alimwaga machozi wakati alipokuwa akipokea Medali kwa niaba ya marehemu Mafisango, aliyefariki dunia wiki iliyopita kwa ajali ya gari maeneo ya Keko, Dar es Salaam, kabla ya kuzikwa kwao, DRC siku tatu baadaye.
  Kiungo wa Simba, Salum Machaku aliitoa Medali aliyokabidhiwa kwenye sherehe hizo kwa marehemu Mafisango.  
  Kaseja, ambaye pia ni Nahodha wa Simba, alinyamaza baada ya kubembelezwa na wachezaji wenzake na kuendelea na shughuli hiyo iliyofana na kuhudhuriwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo.
  Ukumbi pamoja na mapambano yake yaliyowekwa, lakini ulipendeza zaidi kwa mavazi ya mashabiki wa Simba ya rangi nyekundu na nyeupe.
  Meneja wa Global Publishers Limited, Abdallah Mrisho alikabidhi Sh. Milioni 3 kwa Kaseja kama zawadi yao kwa Simba kutokana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.
  Baada ya yote hayo, wachezaji na viongozi wa Simba walifungua shampeni na sherehe ikaanza rasmi- kwa hakika mambo yalikuwa mazuri Dar Live, bendi ya Msongo Ngoma ikianza kutumbuiza, ikiongozwa na mwimbaji wake mkongwe, shabiki maarufu wa Simba, Mzee Muhiddin Mwalimu Gurumo.    
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KASEJA AANGUA KILIO DAR LIVE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top