• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 25, 2012

  BLATTER AKATAA MIKWAJU YA PENALTI, ASEMA ITALETA BALAA


  Sepp Blatter
  Blatter
  RAIS wa FIFA, Sepp Blatter amesema kwamba soka inaweaza kugeuka janga iwapo mechi itaamuliwa kwa mikwaju ya penalti.

  Licha ya kutawala mechi ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ndoto za Bayern Munich kutwaa taji hilo la Ulaya, zilizimwa na Chelsea kwa bahati nasibu ya mikwaju ya penalti Jumamosi ya wiki iliyopita.

  Blatter anaamini uhalisia wa soka unapotea inapofikia mechi inaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, na amesema kwamba ufumbuzi utatafutwa baadaye.

  "Soka inaweza kuwa janga unakwenda kwenye mikwaju ya penalti," Blatter alisema kwa mujibu wa BBC. "Soka haiwezi kuwa ya mmoja kwa mmoja, inapofikia kwenye mikwaju ya penalti soka inapoteza uhalisi wake.

  "Natumai Franz Beckenbauer na Kamati yake ya [FIFA Task Force]  2014 watatuonyesha njia, hata isiwe leo, lakini baadaye."

  Katika jitihada za kurekebisha zaidi mchezo huo, FIFA imetangaza kwamba mechi ya kirafiki kati ya England na Ubelgiji Juni 2, itatumika kufanyia majaribio sheria ya teknolojia kwenye mstari wa lango, ili kujua kama mpira umevuka, au haujavuka mstari.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BLATTER AKATAA MIKWAJU YA PENALTI, ASEMA ITALETA BALAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top