• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 25, 2012

  MARTINEZ ATUA MIAMI KUZUNGUMZA NA WAMILIKI LIVERPOOL


  Roberto Martinez
  Afika Miami kushauriana na matajiri wa Liverpool

  MMILIKI wa klabu ya soka ya Wigan, Dave Whelan amesema Roberto Martinez amefika Miami, Marekani, kushauriana na matajiri wanaomiliki klabu ya Liverpool.
  Whelan alitoa ruhusua wiki iliyopita kwa Martinez kufanya mashauri na timu ya Liverpool, na kuamua ikiwa atajiunga nao kama meneja, na Whelan amempa hadi tarehe 5 Juni kuamua atasalia Wigan, ama atajiunga na Liverpool.
  "Roberto yuko Miami leo, na unaweza kuamua amefika huko kufanya nini [kuzungumza na wamiliki wa Liverpool]," Whelan aliielezea BBC.
  "Yeye ni mtu mwaminifu, na ninatazamia katika kipindi cha saa 48 zijazo aniarifu yaliyoafikiwa."
  Mashauri hayo ya Martinez yanaashiria mazungumzo rasmi yameanza kufanyika katika juhudi za klabu ya Liverpool kumtafuta meneja mpya, baada ya kumfuta kazi Kenny Dalglish tarehe 16 Mei.
  Meneja wa Swansea, Brendan Rodgers, na Frank de Boer wa klabu ya Ajax ya Uholanzi, ni kati ya meneja ambao wamekataa ombi la kuhojiwa kwa kibarua hicho cha klabu ya Anfield.
  Aliyekuwa meneja wa Chelsea zamani, Andre Villas-Boas ni kati ya watu ambao wanafikiriwa huenda wakachaguliwa kuifunza Liverpool.
  Martinez, ambaye alikuwa kocha wa zamani wa Swansea, na mwenye umri wa miaka 38, alikataa kuwa meneja wa Aston Villa msimu uliopita, na hivi sasa yuko likizoni Barbados, hadi Jumanne, na amepewa muda wa siku saba na Whelan kuamua atabaki Wigan au atajiunga na Liverpool.
  Whelan anatumaini hali hiyo ya kutofahamu kinachoendelea itakwisha haraka.
  Aliongezea: "Yuko Carribean, kwa hiyo ni muda wa saa mbili kufika Miami.
  "Ikiwa ataamua kuondoka, na natumaini hatafanya hivyo, basi itanibidi kumtafuta atakayejaza pengo haraka iwezekanavyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MARTINEZ ATUA MIAMI KUZUNGUMZA NA WAMILIKI LIVERPOOL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top