Tetesi za J'mosi magazeti ya Ulaya

BERBATOV ATIMKIA PSGHAZARD

MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Dimitar Berbatov, mwenye umri wa miaka 31, anatarajiwa kuhamia kwa wamwaga fedha lukuki wa Ufaransa, Paris Saint-Germain.
MSHAMBULIAJI wa Ubelgiji, Eden Hazard, ambaye anatakiwa Manchester City na Chelsea, ameamua kusaini Manchester United, kwa mujibu wa vyanzo kutoka Ufaransa. Hazard, mwenye umri wa miaka 21, tayari amethibitisha anakwenda Ligi Kuu ya England, baada ya msimu mzuri na Lille.
KLABU ya Manchester United imekwama kumpata kiungo Mjapan Shinji Kagawa mwenye umri wa miaka 23 kwa dau la pauni Milioni 12.8 kutoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Heerenveen striker Bas Dost
Mshambuliaji wa Heerenveen, Bas Dost.
KOCHA Sir Alex Ferguson anataka kusajili kwa pauni Milioni 4, kinda lenye kipaji cha hali ya juu la Crewe, Nick Powell, mwenye umri wa miaka 18.
KLABU iliyorejea Ligi Kuu msimu ujao, West Ham imetoa ofa ya pauni Milioni 7 kwa mshambuliaji wa Heerenveen, Bas Dost, mwenye umri wa miaka 22, ambaye amefunga mabao 32 katika mechi 34 za ligi na klabu yake msimu huu.
KLABU ya Everton imefungua maongezi na mshambuliaji wa kimataifa wa Norway, anayaechezea klabu ya Lillestrom, Bjorn Bergmann Sigurdarson, mwenye umri wa miaka 21, kwa dau la pauni Milioni 3.
KOCHA Tony Pulis anataka kumsajili Matt Jarvis, mwenye umri wa miaka 26, ingawa kocha huyo wa Stoke anamthamanisha winga huyo kwa nusu ya dau linalotakiwa na klabu yake, Wolves pauni Milioni 10.
NYOTA wa Fulham, Clint Dempsey, mwenye umri wa miaka 29, amezua hofu katika klabu yake, baada ya kuliambia jarida la Marekani, Sports Illustrated kwamba anataka kucheza Ligi ya Mabingwa.
KLABU ya Huddersfield imezionya klabu zinazommezea mate mshambuliaji wake hatari, Jordan Rhodes, mwenye umri wa miaka 22, zikiwemo Fulham, Everton na Aston Villa, kwamba ataruhusiwa kuondoka kwa dau la pauni Milioni 8 tu.
KLABU ya DC United inajipanga kumsajili beki wa Tottenham, Ryan Nelsen, mwenye umri wa miaka 34, kwa mara ya pili. Nelsen alijiunga na Blackburn baada ya kucheza Ligi Kuu ya Marekani, Major League Soccer.
KLABU ya Newcastle ipo kwenye vita kali na Porto katika kuwania saini ya beki wa kulia wa FC Twente, Roberto Rosales, mwenye umri wa miaka 23, kwa dau la pauni Milioni 3, kwa mujibu wa wakala wa kimataifa wa Venezuela.
KLABU ya Leicester ipo karibu kukamilisha mpango wa kubadilishana wachezaji na Celtic, ambao ni beki wa kati wa England, Kelvin Wilson, mwenye umri wa miaka 26 na Matt Mills, mwenye miaka 25, watakayemtoa.

BRUCE KUREJEA WIGAN

KLABU ya Wigan itamsomesha kocha Steve Bruce arejee kupiga kazi Uwanja wa DW kwa mara ya tatu, iwapo Roberto Martinez anayetakiwa na Liverpool, ataondoka.
KOCHA wa England, Roy Hodgson anajiandaa kucheza bahati nasibu kwa kumchukua mshambuliaji Danny Welbeck kwenda naye kwenye Fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012, ingawa hayuko fiti kwa asilimia 100. Mshambuliaji huyo wa Manchester United atakosa mechi ya kirafiki na Norway kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu na hatarajiwi kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kabla ya Jumanne ijayo, wakati Hodgson atakapotakiwa lazima awe amekwishawasilisha kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 kwa ajili ya fainali hizo za Euro zinazoandaliwa kwa pamoja na Poland na Ukraine.

RAFIKI wa siku nyingi wa kocha 
Sir Alex Ferguson, Dave Whelan, Mmiliki wa klabu ya Wigan, amesema kocha huyo wa Manchester United manager, mwenye umri wa miaka 70, atastaafu mwishoni mwa msimu ujao.Habari kamili: the Times (subscription required) 

MANCINI KUMTEMA MWANAWE MAN CITY
KOCHA wa Manchester City, Roberto Mancini anatarajiwa kuonyesha msimamo wake kwa kumpiga chini mwanawe, Andrea, mwenye umri wa miaka 19 kwenye timu hiyo.