• HABARI MPYA

    Wednesday, May 23, 2012

    MWANAMUZIKI WA ZAMANI ANAUMWA, ANAHITAJI MSAADA



    Waraka huu nimetumiwa na mwanamuziki mahiri Benno Villa Anthony.................Mkuu, kwanza kabisa namwomba Mwenyezi Mungu akujalie roho ya uvumilivu ktk kufuatilia taarifa hii. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilikuwa na kipindi cha mahojiano na Manju wa muziki na mtangazaji wa TBC, komredi Masuud Masuud. Kwa vile kipindi kilirudiwarudiwa na huku Manju akitamka namba yangu ya simu, wengi waliinukuu, na kati ya hao walioinyaka ni Mzee John Mbulla, aliyekuwa mpiga sax wa Atomic Jazz. Mzee huyu kwa sasa kweli anaumwa sana. Zaidi ni maradhi ya macho, haoni. Kumbe kwao ni Mpwapwa ila kwa sasa anahifadhiwa na diwani wa Kibaigwa, Ndugu Richard Kapinye.......0717  303070. Baada ya kusikia kuwa wasanii wanachangiana ili kupata tiba, Diwani huyo alinipigia na nikazungumza nao wote wawili. Wameniomba nikupe taarifa hii ili uitoe kwenye vyombo vya habari, ikiwezekana apate msaada wa tiba. Diwani anasema kuwa John akipata operation ya macho atapona na kuanza kujitegemea maana nguvu bado anazo. KUMBUKA...Mzee John Mbulla ndiye aliyepiga Saxaphone kwenye wimbo wa "TANZANIA YETU NDIYO NCHI YA KUSIFIWA", wakati Mbaraka Mweshehe alipojiunga na Atomic Jazz  kwa muda..............Mkuu Kitime, Nina uhakika kama wana Media wakimtembelea na kutoa habari zake, naamini wengi wataguswa na kumsaidia.  Natanguliza shukrani zangu za awali. Asante Mkuu.

    SOURCE: KIJIWE CHA KITIME
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MWANAMUZIKI WA ZAMANI ANAUMWA, ANAHITAJI MSAADA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top