Tetesi za Alhamisi magazeti Ulaya

ROONEY ATAKIWA KWA EURO MILIONI 150 UFARANSA

KLABU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa inajiandaa kufanya kufuru mbaya- kutoa dau la Euro Milioni 150 kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
KLABU za Tottenham na Chelsea zinajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Newcastle, Demba Ba, ambaye amepewa ruhusa binafsi ya kuhama kwa dau la pauni la Milioni 7.
KLABU ya Chelsea ipo karibuni kumnasa kwa dau la pauni Milioni 40, mshambuliaji wa Porto, Hulk, mwenye umri wa miaka 25, huku mazungumzo yakitarajiwa kuendelea baadaye wiki hii.
KLABUA za Manchester United, Chelsea na Arsenal zinamfuatilia kinda wa umri wa miaka 22 wa Ukraine, kiungo wa Dnipro, Yevhen Konoplyanka.
Rafael Van der Vaart
Rafael van der Vaart.
MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Rafael van der Vaart anatazamiwa kuondoka White Hart Lane baada ya Schalke  kuonyesha nia ya kumchukua Mholanzi huyo kwa dau la pauni Milioni 10.
KLABU za Tottenham na Newcastle zimeingia kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa Manchester City, Adam Johnson.
WAPINZANI wa Kaskazini kwa London, Arsenal na Tottenham zina mpango wa kumsajili kiungo wa Sochaux, Marvin Martin baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kusema anataka kuondoka Ufaransa.
KLABU ya Arsenal inataka kumpa ofa Salomon Kalou kubaki katika Ligi Kuu ya England, baada ya kutemwa na klabu yake ya sasa, Chelsea, huku kukiwa kuna habari anataka kwenda Schalke.
KLABU ya Newcastle imeripotiwa kutenga dau la kati ya pauni  500,000 na Milioni 1 kumnasa kinda wa Coventry, Gael Bigirimana, mwenye umri wa miaka 18.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill yuko tayari kumnasa Msenegali wa Wigan, kiungo nyota Mohamed Diame, mwenye umri wa miaka 24.

ATEMWA KIKOSI CHA EURO KWA KUSHINDWA WIMBO WA TAIFA

KOCHA Mserbia, Sinisa Mihajlovic amemtema  Adem Ljajic baada ya mshambuliaji huyo kushindwa kuimba wimbo wa taifa kabla ya mechi waliyofungwa 2-0 na Hispania Jumamosi.