• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 25, 2012

  COLE AANDALIWA MKATABA MPYA MNONO CHELSEA SAWA NA WA TORRES


  UEFA Champions - FC Bayern Muenchen vs Chelsea FC, Ashley Cole
  Ashley Cole
  EXCLUSIVE
  By Wayne Veysey | Chief Correspondent

  KLABU ya Chelsea, iko tayari kumpa ofa ya mkataba mpya Ashley Cole ambao utamuweka Stamford Bridge kwa kipindi chote kilchobaki cha maisha yake ya soka.
  Beki huyo amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake wa sasa na klabu hiyo inataka kumfunga kwa mkataba mpya mwanzoni mwa msimu ujao, kwa mazungumzo ambayo yataanza hivi karibuni, baada ya beki huyo wa kushoto kuonyesha soka ya nguvu msimu huu, akitoa mchango mkubwa kwa timu kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa.
  Chanzo cha habari, kimeiambia Goal.com, ambako BIN ZUBEIRY imeipata habari hii, kwamba beki huyo mwenye umri wa miaka 31 atapewa mkataba wa makia mitatu na kuingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa vizuri katika klabu hiyo, sambamba na akina  John Terry, Frank Lampard na Fernando Torres.
  Mshahara wake wa sasa inasemekana ni kiasi cha pauni 120,000 kwa wiki, wakati Barcelona ni miongoni mwa klabu ambazo zinamtaka sana Cole na kwa sasa inasikilizia tu kama Chelsea itashindwana naye, iingie msituni kusaka saini ya mchezaji huyo, aliyesajiliwa Stamford Bridge katika mazingira ya utatanishi kutoka Arsenal mwaka 2006.
  Hadi sasa hakuna dalili kwamba Cole anataka kuondoka London na baada ya kumaliza msimu na mataji mawili, kwa sasa yuko likizo Los Angeles, Marekani kabla ya kujiunga na timu ya taifa ya England wiki ijayo kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Ubelgiji Juni 2, mwaka huu.
  Pamoja na kurefusha maisha ya Cole, Stamford Bridge, pia Chelsea inataka kuwaongezea mikataba Michael Essien, Florent Malouda na Frank Lampard, ambao wanamaliza 2013.
  Kama BIN ZUBEIRY ilivyoinukuu Goal.com Jumatano kwamba Salomon Kalou anaweza kutemwa, sasa suala lake litatatuliwa wiki ijayo, wakati Jose Bosingwa anajiandaa kutemwa licha ya kuwa beki chaguo la kwanza kulia katika kikosi kilichomaliza msimu na mataji mawili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: COLE AANDALIWA MKATABA MPYA MNONO CHELSEA SAWA NA WA TORRES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top