• HABARI MPYA

  Wednesday, May 23, 2012

  PIGO LINGINE TAIFA STARS, ULI MABAO AUMIA KIFUNDO CHA MGUU


  Ulimwengu katika uzi wa Brazil

  TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu naye kuumia kifundo cha mguu.
  Kuumia kwa Ulimwengu anayekipga katika klabu ya TP Mazembe ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunafa timu hiyo kufikisha majeruhi wawili ambapo jana, kiungo wake Nurdin Bakari alichanika nyama za paja hali itakayomlazimu kukaa nje ya dimba kwa siku saba.
  Daktari wa Stars, Mwanandi Mwankemwa ameiambia mamapipiro blog Ulimwengu alipata maumivu hayo wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
  Alisema kutokana na maumivu hayo, Ulimwengu naye ataukjosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
  Stars inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen akisaidiwa na Mzalendo Sylvestre Marsh imepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma jijini  Dar es Salaam ikijiandaa mechi yake  ya mchujo kufuzu Kombe la Dunia  hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa  Abidjan  Juni 2 mwaka huu. 

  SOURCE: DINA ISMAIL (http/mamapipiro.blogspot.com)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PIGO LINGINE TAIFA STARS, ULI MABAO AUMIA KIFUNDO CHA MGUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top