• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 25, 2012

  HATIMA YA YANGA SASA IPO KWA ALEX MGONGOLWA


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linatafakari mustakabali wa Yanga, kufuatia Wajumbe kadhaa wa Kamati ya Utendaji ya Yanga akiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga kujiuzulu.
  Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniphace Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, Kamati ya Uchaguzi ya Yanga imeliandikia barua shirikisho hilo, ikitaka mwongozo juu ya hilo.
  Wambura amesema kwamba, kwa kuzingatia hilo, TFF imepeleka suala hilo kwa Kamati yake ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ili itoe maoni yake kisheria ya nini kinafanyike kuhakikisha Yanga inaendelea na shughuli zake kama kawaida.
  Amesema Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti wake, Alex Mgongolwa (pichani) inatarajia kukutana leo jioni kushughulikia suala hilo na baadaye Kamati ya Uchaguzi ya Yanga pamoja na Kamati ya Uchaguzi ya TFF zitapewa maelekezo ya kufanya kwa kuzingatia taratibu zilizopo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HATIMA YA YANGA SASA IPO KWA ALEX MGONGOLWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top