• HABARI MPYA

  Tuesday, May 29, 2012

  MAMA VUVUZELA WA MASHAUZI AIPUA NGOMA MPYA KALI KINOMA

  MWIMBAJI nyota wa kundi la Mashauzi Classic, Aisha Othman 'Mama Vuvuzela' ameibuka na wimbo mpya uitwao, La Mungu Halina Mwamuzi ambao unatarajiwa kuanza kusikika kwenye vituo mbalimbali vya Radio nchini wakati wowote kuanzia sasa.
  Aisha, ameiambia BIN ZUBEIRY mchana huu kwamba, wimbo huo umetungwa na Thabit Abdul ambaye ni Mkurugenzi wa bendi hiyo na umerekodiwa katika studio za Sound Crafters, chini ya mtaalamu Enrico.
  "Wapenzi na mashabiki wangu na mashabiki wa Mashauzi Classic na wapenzi wa Taarabu kwa ujumla, wakae mkao wa kula kupokea kitu kipya kitamu, mtoto nimetulia humo ndani, nimefanya mambo makubwa,"alisema Aisha.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAMA VUVUZELA WA MASHAUZI AIPUA NGOMA MPYA KALI KINOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top