• HABARI MPYA

  Jumapili, Mei 27, 2012

  MAKALA ABWAGA MANYANGA SIMBA, KUWAPIGA TAFU NA YANGA


  NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. Amos Makalla amesema amejitoa kwenye Kamati za Simba baada ya kuteuliwa kuwa Waziri na kuanzia sasa atakuwa akisaidia klabu zote nchini.
  Makalla amesema hayo katika sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu ya Bara za Simba kwenye ukumbi wa Dar Live, Mbagala jioni ya leo.
  Pamoja na hayo, Makalla amesema amechangia sana mafanikio ya Simba msimu huu, akiwa kwenye Kamati aliyoteuliwa na ameutaka uongozi wa klabu hiyo kutobweteka na mafanikio hayo na badala yake kujipanga vizuri ili kufanya vizuri zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAKALA ABWAGA MANYANGA SIMBA, KUWAPIGA TAFU NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top