• HABARI MPYA

  Ijumaa, Mei 25, 2012

  KILIMANJARO PREMIUM LAGER KUENDELEA KUDHAMINI KOMBE LA TAIFA

  George Kavishe, Meneja wa Kilimanjaro Beer
  Gaudence Mwaikimba, mfungaji bora wa taifa Cup msimu
  uliopita akiwa na mabingwa watetezi Mbeya
  MENEJA wa Bia ya Kilimajaro Premium Lager, George Kavishe amesema kwamba pamoja na kuingia mkataba wa kuidhamini timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, lakini wataendelea pia kudhamini mashindano ya Kombe la Taifa, Kili Taifa Cup.
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY jana usiku katika mahojiano maalum, Nyumbani Lounge, Oysterbay, Dar es Salaam, Kavishe alisema kwamba Kilimanjaro Premium Lager bado ni wadhamini wa Taifa Cup na mwaka huu itafanyika kama kawaida.
  Hata hivyo, alipoulizwa juu ya ukimya wa maandalizi hadi sasa, Kavishe alisema; “Sisi tunawasubiri TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), wao ndio wanatakiwa kutupa mwongozo, sisi ni wadhamini tu, tunawezesha, ila mipango yote na nini, ni TFF wao wenyewe,”alisema Kavishe ambaye jana bia yake ilifanya pati la uzinduzi wa kampeni ya Kilimanjaro Premium Lager 100% TZ Flava kwenye ukumni wa Nyumbani Lounge.
  Kumekuwa na wasiwasi wa Kombe la Taifa ama kutofanyika kabisa mwaka huu, au kufanyika bila ya udhamini, baada ya Kilimanjaro Premium Lager ambao pia ni wadhamini wa klabu za Simba na Yanga, kuingia mkataba wa kuidhamini Taifa Stars, ambayo awali ilikuwa inadhamini na bia ya Serengeti Premium Lager.
  Lakini kauli hii ya Kavishe inakuja kuondoa wasiwasi huo na mikoa sasa inaweza kuendelea na maandalizi yake kama kawaida.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO PREMIUM LAGER KUENDELEA KUDHAMINI KOMBE LA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top