Tetesi za J'tano magazeti ya Ulaya

MANCHESTER CITY SASA KUMSAJILI WESLEY SNEIJDER

KLABU ya Manchester City inaweza kubomoa benki na kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, anayekipiga Inter Milan ya Italia, Wesley Sneijder, mwenye umri wa miaka 27.
KLABU ya Manchester United kwa kiasi kikubwa ipo karibu kumnasa kwa dau la pauni Milioni 12, kiungo wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 23, Shinji Kagawa.
Manchester City's Adam Johnson
Manchester United inamtaka Adam Johnson
KLABU ya Manchester United imetega rada zake kwa ajili ya kumnasa winga wa wapinzani wao, Manchester City, Adam Johnson mwenye umri wa miaka 24.
KOCHA wa Sunderland, Martin O'Neill pia anamtolea macho Adam Johnson na anataka kumpa nafasi ya kuonyesha uwezo wake ili arejeshwe kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.
KLABU za Manchester United na Manchester City, zote zinamtolea macho Papiss Cisse, ambaye amefunga mabao 13 katika mechi 14 za Ligi Kuu tangu ajiunge na Newcastle Januari, mwaka huu.
KLABU ya Rennes imewaambia Arsenal na Inter Milan wanaweza kusahau kumsajili kinda wao wa miaka 21, Yann M'Vila hadi baada ya Euro 2012, ili kutoa nafasi kwa kiungo huyo kuzivutia klabu nyingi zaidi katika dirisha hili la usajili.
MCHEZAJI wa klabu ya Real Madrid, Joselu, mwenye umri wa miaka 22, anaweza kuanza mpango wa kuhamishia maskani yake katika Ligi Kuu ya England.
KLABU ya Everton inataka kumsajili mshambuliaji wa Benfica, Oscar Cardozo, mwenye umri wa miaka 29, ahamishie cheche zake Uwanja wa Goodison Park.
MCHEZAJI Andy Johnson anaweza kuwa mchezaji mwingine mwenye jina kubwa kuhama Ligi Kuu ya England kwenda kucheza Pro League, baada ya wakala wa mshambuliaji huyo wa Fulham kuthibitisha kuna klabu zinamataka za Halme za Kiarabu (UAE).
KLABU ya Liverpool itabidi kwanza ipambane na Galatasaray, kama inamtaka kiungo wa Real Madrid, mwenye umri wa miaka 29, Hamit Altintop.
MCHEZAJI Ledley King atakuwa huru mwezi ujao, lakini anajiandaa kupokea mkataba mpya wa miezi 12 Tottenham, wakati atakapoketi chini na uongozi wa klabu hiyo wiki hii kujadili kujadili nao.

LIVERPOOL SASA YAMGEUKIA KOCHA WA SWANSEA CITY

KLABU ya Liverpool ina matumaini kufufua mpango wa kumchukua kocha wa Swansea, Brendan Rodgers awe kocha wao mpya na Louis van Gaal awe Mkurugenzi wao wa Michezo.
Wigan manager Roberto Martinez
Roberto Martinez sasa anaifikiria Aston Villa
SASA ni dhahiri Liverpool imeshindwa kumpata kocha Roberto Martinez, kutokana na kocha huyo wa Wigan, kuhamishia nguvu zake katika mpango wa kujiunga na Aston Villa.
KWA dau la pauni Milioni 15, Brian McDermott anaweza kutua Reading, baada ya klabu hiyo kuchukuliwa na bilionea wa Kirusi, Anton Zingarevich.
MCHEZAJI Phil Jones anatarajia kuwa na nafasi nzuri ya kujiimarisha katika kikosi cha England, kama beki wa kulia chaguo la kwanza katika michuano ya Euro 2012, kutokana na kocha Roy Hodgson kumtilia shaka Glen Johnson katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ubelgiji Jumamosi.
ANDY CARROL YUKO SAWA
MASHABIKI wa England wanatumaini Andy Carroll yuko sawa sawa hivi sasa kwa mechi za kimataifa, kuliko alivyokuwa timu za vijana, baada ya mshambuliaji huyo wa Liverpool kuonekana kuimarika siku za karibuni.