Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia bao pili Real Madrid dakika ya 80 kufuatia kuingia akitokea benchi kipindi cha pili timu yake ikishinda 3-1 dhidi ya wenyeji, Barcelona Uwanja wa Camp Nou kwenye mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania usiku wa jana. Mabao mengine ya Real yalifungwa na Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 50 na Marco Asensio dakika ya 90, wakati la Barca lilifungwa na Lionel Messi dakika ya 77 kwa penalti. Ronaldo alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 82, kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili njano, ya kwanza kwa kuvua shati wakati wa kushangilia na ya pili kwa kujiangusha PICHA ZAIDI GONGA HAPA
UNESCO yafunga mafuzo ya Mafundi Mitambo wa Radio za jamii 25
-
*Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo akizungumza kuhusu
UNESCO i...
4 hours ago
0 comments:
Post a Comment