// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Monday, July 08, 2024

  SIMBA SC YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU


  KIKOSI cha Simba SC kimeondoka leo jioni Jijini Dar es Salaam kwenda mjini Ismaili nchini Misri kuweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya.
  VIDEO: AHMED ALLY AKIZUNGUMZIA SAFARI YA MISRI 

  Simba SC inaondoka baada ya kutambulisha wachezaji wapya 12, ambao ni mabeki, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya DRC, wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
  Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
  Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC na Rais wa heshima wa klabu hiyo, Mohamed 'Mo' Dewji jana alikutana na wachezaji na makocha kwa mazungumzo kabla ya timu kuondoka.
  VIDEO: MO DEWJI AKIZUNGUMZA NA WACHEZAJI JANA
  Aidha, Simba SC imeleta Kocha Mkuu mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids (43) raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mualgeria Abdelhak Benchika aliyeondoka April 28, mwaka huu.
  Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
  VIDEO: MAKOCHA WAPYA WALIPOKUTANA NA VIONGOZI JANA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAENDA MISRI KUWEKA KAMBI YA KUJIANDAA NA MSIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top