• HABARI MPYA

  Monday, July 01, 2024

  CLATOUS CHOTA CHAMA MCHEZAJI WA KWANZA MPYA YANGA SC


  KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo Mzambia, Clatous Chota Chama kuwa mchezaji wake mpya wa kwanza kielekea msimu ujao.
  Chama (33), ambaye amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya Taifa ya Zambia tangu mwaka 2015 anajiunga na Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kws vipindi viwili kuanzia mwaka 2018
  Aliwasili Simba SC mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya kwao, akacheza hadi mwaka 2021 alipouzwa RS Berkane ya Morocco, kabla ya kurejea Msimbazi mwaka 2022 na sasa anahamishia huduma zake Jangwani.
  Kisoka Chama aliibukia ZESCO United ya kwao mwaka 2016, kabla ya kuhamia Al Ittihad ya Mısri mwaka 2017 ambako alicheza kwa miezi kadhaa na kurejea Zambia kujiunga na Lusaka Dynamos.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CLATOUS CHOTA CHAMA MCHEZAJI WA KWANZA MPYA YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top