• HABARI MPYA

  Monday, July 08, 2024

  RASMI YUSUPH ALLY KAGOMA NI MCHEZAJI MPYA WA SIMBA SC


  KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo wa ulinzi, Yusuph Ally Kagoma (28) kuwa mchezaji mpya kutoka Singida Big Stars kuwa mchezaji wake mpya wa 12 kuelekea msimu ujao.
  Wachezaji wengine wapya 11 Simba SC ni mabeki, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya DRC, wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
  Wengine ni kiungo wa ulinzi, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, kiungo mzawa Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma na winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe.
  Wapya wengine ni kiungo mshambuliaji, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia na  washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
  Aidha, Simba SC imeleta Kocha Mkuu mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids (43) raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mualgeria Abdelhak Benchika aliyeondoka April 28, mwaka huu.
  Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
  Kikosi kinatarajiwa kuondoka Jumatatu kwenda mjini Ismailia nchini Misri kuweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASMI YUSUPH ALLY KAGOMA NI MCHEZAJI MPYA WA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top