• HABARI MPYA

  Thursday, July 11, 2024

  YANGA KUANZA NA VITAL’O, AZAM NA APR LİGİ YA MABINGWA AFRIKA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Vital’O ya Burundi, wakati Azam FC itaanza na APR ya Rwanda katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Yanga itaanzia ugenini na Azam FC itaanzia nyumbani mechi za kwanza zitachezwa kati kati ya Agosti 16 na 18, kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 23 na 25.
  Kwa upande wao JKU ya Zanzibar wataanzia nyumbani dhidi ya Pyramids ya Mısri.
  Yanga ikiitoa Vital’O itakutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia na Azam FC ikiitoa APR itakutana na mshindi kati ya JKU na Pyramids ya Mısri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA KUANZA NA VITAL’O, AZAM NA APR LİGİ YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top