// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA BABACAR SARR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA BABACAR SARR - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Wednesday, July 10, 2024

  SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA BABACAR SARR


  KLABU ya Simba imeachana na kiungo Msenegal, Babacar Sarr (33) baada ya nusu msimu tangu awasili Januari mwaka huu kutoka US Monastir ya Tunisia.
  Huyo anakuwa mchezaji wa nane kuachwa Simba baada ya mabeki, Mkongo Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji, Sadio Kanoute wa Mali na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.
  Aidha, Simba imesajili wachezaji wapya 12, ambao ni mabeki, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya DRC, wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
  Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia.
  Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
  Simba SC pia imeleta Kocha Mkuu mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids (43) raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mualgeria Abdelhak Benchika aliyeondoka April 28, mwaka huu.
  Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA BABACAR SARR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top