• HABARI MPYA

  Wednesday, July 03, 2024

  CHAMA AWAAGA RASMI SIMBA NI KUJITAMBULISHA YEYE SASA NI YANGA


  KIUNGO Mzambia, Clatous Chota Chama ameandika wraka wa kuiaga klabu ya Simba kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya kujiunga na mahasimu, Yanga.
  “Miaka sita iliyopita nilikuja kama mgeni. Mkanipa nafasi na changamoto ya kuwa toleo bora zaidi kwangu.
  Tuliiteka ardhi hii kwa pamoja, tukajitanua hadi sehemu nyingine za Afrika, na mengine ni historia.
  Baada ya miaka sita ya furaha kubwa, kiburi, na malengo, hatima zetu zilizounganishwa zinachukua mkondo tofauti.
  Sina chochote, isipokuwa heshima kwa kila mmoja wenu kwa upendo na sapoti mliyonipa miaka yote na hakuna anayeweza kubadilisha historia tuliyotengeneza pamoja.
  Wanasema; “Show haijaisha mpaka ‘Mama Kibonge’ aimbe nami ninaamini wimbo huo una thamani kwaenu.
  Nawatakia kila la kheri na tutaendelea kuonana,” ameandika Chama sambamba na kujitambulisha kama mchezaji wa Yanga katika akaunti yake hiyo.


  Chama (33), ambaye amekuwa mchezaji muhimu wa timu ya Taifa ya Zambia tangu mwaka 2015 anajiunga na Yanga baada ya kuitumikia Simba SC kws vipindi viwili kuanzia mwaka 2018.
  Aliwasili Simba SC mwaka 2018 akitokea Lusaka Dynamos ya kwao, akacheza hadi mwaka 2021 alipouzwa RS Berkane ya Morocco, kabla ya kurejea Msimbazi mwaka 2022 na sasa anahamishia huduma zake Jangwani.
  Kisoka Chama aliibukia ZESCO United ya kwao mwaka 2016, kabla ya kuhamia Al Ittihad ya Mısri mwaka 2017 ambako alicheza kwa miezi kadhaa na kurejea Zambia kujiunga na Lusaka Dynamos.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA AWAAGA RASMI SIMBA NI KUJITAMBULISHA YEYE SASA NI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top