• HABARI MPYA

  Wednesday, July 10, 2024

  SINGIDA BIG STARS YAANZA VIBAYA KOMBE LA KAGAME, YAPIGWA 1-0 CHAMAZI


  TIMU ya Singida Big Stars jana ilianza vibaya michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuchapwa 1-0 na mabingwa wa zamani, APR ya Rwanda katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Mechi ya Kundi C iliyotangulia jana, SC Villa ya Uganda iltoka sare ya bila kufungana na El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini.
  Mapema katika mechi za Kundi zilizotangulia, Coastal Union ilishinda 1-0 dhidi ya Dekadaha ya Somalia, bao pekee la kiungo Ramadhani Mwenda dakika ya 45, wakati Hay Al Wadi ya Sudan iliichapa JKU ya Zanzibar 1-0 bao pekee la Jebril Mohamed Uwanja wa KMC, Mwenge Jijini Dar es Salaam. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SINGIDA BIG STARS YAANZA VIBAYA KOMBE LA KAGAME, YAPIGWA 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top