• HABARI MPYA

  Friday, July 05, 2024

  SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI WA GEITA GOLD


  KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji Valentino Mashaka Kusengama (22) kuwa mchezaji wake mpya r timu ya Geita Gold ambayo imeshuka daraja.
  Valentino Mashaka Kusengama  anakuwa mchezaji mpya wa saba Simba SC baada ya mabeki wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
  Wengine ni winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya Zambia na washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI WA GEITA GOLD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top