• HABARI MPYA

  Wednesday, July 03, 2024

  UHOLANZI NA UTURUKI ZAKAMILISHA ROBO FAINALI EURO 2024


  TIMU za Uholanzi na Uturuki zimefanikiwa kutinga Robo Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya kuzitoa Romania na Austria jana nchini Ujerumani.
  Ilianza Uholanzi kuitandika Romania 3-0, mabao ya washambuliaji, Cody Mathès Gakpo wa Liverpool dakika ya 20 na Donyell Malen wa Borussia Dortmund mawili dakika ya 83 na 90 Uwanja wa Allianz Arena. Jijini Münich.
  Naye beki wa Al-Ahli  ya Saudi Arabia, Merih Demiral alifunga mabao yote, dakika ya kwanza na ya 59, Uturuki ikiichapa Austria 2-1 Uwanja wa Red Bull Arena, Jijini Leipzig. 
  Bao la kufuatia machozi la Austria lilifungwa na winga wa SC Freiburg, Michael Gregoritsch dakika ya 66 na sasa Uturuki itakutana na Uholanzi katika Robo Fainali Jumamosi Uwanja wa Olympia Jijini Berlin.
  Robo Fainali nyingine ni Ijumaa Hispania na Ujerumani na Ureno Ufaransa, wakati England na Uswisi nazo pia zitaumana Jumamosi.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UHOLANZI NA UTURUKI ZAKAMILISHA ROBO FAINALI EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top